RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema hatua ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kufungua Ubalozi mdogo hapa Zanzibar, itaendeleza kasi katika kukuza uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya nchi hizo mbili.

Dk. Mwinyi amesema hayo Ikulu Zanzibar, alipozungumza na Konseli Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Saleh Ahmeid Alhemeir aliefika kwa ajili ya kujitambulisha.

Alisema hatua ya nchi hiyo kufungua Ubalozi mdogo hapa Zanzibar kutatoa msukumo katika utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo ilioanzishwa pamoja na ile inayolengwa kuanzishwa siku za usoni.

Alisema ni matarajio yake kuwa kupitia Konseli Mkuu Alhemeir, miradi mbali mbali inayotekelezwa na nchi hiyo kupitia taaisi na mashirika ya fedha ya nchi hiyo itafanikishwa.

Nae, Konseli Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu hapa Zanzibar Saleh Ahmeid Alhemeir alisema hatua ya UEA kufungua Ubalozi mdogo hapa Zanzibar itaaongeza kasi ya mahirikiano na hivyo akaahidi kufuatilia miradi mbali mbayo nchi hiyo imelenga ikisaidia Zanzibar.

Aidha, alisema atahakikisha anasimamia kikamilifu ujenzi wa Ofisi za Ubalozi mdogo wa nchi hiyo hapa Zanzibar.