Media » News and Events

Dk. Hussein Ali Mwinyi ameungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan katika hitimisho la uzinduzi wa Filamu ya ‘The Royal Tours’

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi leo ameungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan katika hitimisho la uzinduzi wa Filamu ya ‘The Royal Tours’ uliofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam. 

Akizindua filamu hiyo Mama Samia aliwataka Watanzania kujitayarisha na kuwa tayari kupokea wimbi kubwa la watalii wanaotarajiwa kuja nchini baada ya kuhamasika kutokana na filamu hiyo.

Alisema filamu hiyo itaitangaza vyema Tanzania Ulimwenguni kote na hivyo kutoa fursa kwa watalii na wawekezaji wa sekta ya Utalii kuja nchini kuwekeza, kutokana na vianzio mbalio mbali vilivyopo, ikiwemo mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na utamaduni wa Watanzania kupitia makabila mbali mbali.

Aidha, alisema ustawi bora wa Misitu mikubwa iliopo nchini utaliwezesha Taifa kupata fedha nyingi kutokana na rasilimali hiyo ya misitu.

Mama Samia alimpongeza Dk. Mwinyin kwa kushiriki vyema katika filamu hiyo, sambamba na hatua yake ya uzinduzi wa filamu hiyo uliofanyika Zanzibar Mei 7, mwaka huu.

Viongozi mbali mbali wa kitaifa, akiwemo Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, Wake wa Viongozi wakuu, Spika wa Bunge Dk. Tulia Akson, Mabalozi pamoja na viongozi mbali mbali wa Chama (CCM) na Serikali walishiriki