MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amewaahidi viongozi na wanachama wa Maskani ya Kachorora kushirikiana nao kukijenga chama kiuchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla.Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na viongozi na wanachama wa maskani hiyo waliofika kujitambulisha na kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Zanzibar.

Alisema Chama kina mkataba na wananchi ambao ni utekelezwaji wa Ilani ya uchaguzi ya chama cha Mapinduzi na kueleza kuelekea mwaka 2025 watakua na jukumu la kuwaeleza wananchi hao mambo waliyoyafanya kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake.Aidha, Dk. Mwinyi alieleza hatua iliyofikiwa ndani ya kipindi cha miaka miwili cha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, awamu ya nane haipo vibaya na matumaini ni makubwa miaka mitano ijayo. Aliwahakikishia wananchi na wanachama cha CCM ndani ya kipindi cha miaka mitano, miradi mikubwa yote iliyoahidiwa itakamilika.

“Tuna makataba na wananchi mkataba ambao ni Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi, tunakoelekea mwaka 2025, tutakua na jukumu la kusema yepi katika Ilani ya Uchaguzi tumeyatekeleza, hapo tutakua na haki ya kuomba tena kura” Alieleza Makamu Mwenyekiti huyo.Aidha, Dk. Mwinyi alieleza hatua iliyofikiwa ndani ya kipindi cha miaka miwili cha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, awamu ya nane haipo vibaya na yanaonesha matumaini ya miaka mitano ijayo.Hata hivyo, aliwahakikishia wananchi na wanachama cha CCM ndani ya kipindi cha miaka mitano, miradi mikubwa yote iliyoahidiwa itakamilika.

Akizungumzia masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia mfuko wa Uviko 19,  Rais Dk. Mwinyi alieleza suala hilo pia limetajwa kwenye Ilani ya uchaguzi na kusema kuwa ingawa sio watu wote watawezeshwa wakati mmoja lakini alieleza ni suala linalotekelewa kwa awamu na aliwaahidi kila mwananchi atawezeshwa kwa mijibu wa awamu ya fedha zitakavyotoka.Hivyo, aliwaeleza wanamaskani hao kuisaidiwa serikali kuwaelimisha wananchi juu ya dhamira yake njema kwao na kuongeza kuwa kiasi cha shilingi bilioni 16 tayari zimetolewa kwa wananchi awamu ya kwanza na shilingi milioni mbili zimeanzwa kurejeshwa ili kufanya mzunguruko wa fedha hizo.

Dk. Mwinyi aliieleza maskani hiyo kushirikianao nao kwenye ujenzi mzima wa chama na kuwaambia kwamba amedhamiria kukijenga kwa miundombinu imara kuanzia ngazi na shehia hadi taifa kwa kuzimarisha ofisi kwa vifaa vya kisasa pamoja na kuwawezesha watendaji wake.Aliwaeleza wanamaskani hao dhamira yake ya kukijenga chama kwa vifaa vya kisasa vikiwemo komputa, mashine ya fotokopi, na vyombo vya usafiri   pamoja na kuwezesha maslahi ya watendaji wake badala ya kufanya kazi za chama kwa kujitolea.                                                       
                                                                                                                                                                                                                                                                                         
Mapema akizungumza kwenye hafla hiyo, Katibu wa tawi hilo Said Shabaan Said, alimueleza Mamamu Mwenyekiti huyo, kwamba Chama Cha Mapinduzi daima kinaungamkono juhudi za Serikali na kueleza kwamba wamekuwa wakifuatilia shughuli za Serikali zinazofanywa na uongozi wa awamu ya nane na kuongeza kuwa wanaridhishwa kwa kila hatua ya uongozi huo.Aidha, wanachama hao walieleza kuiridhishwa na uongozi wa Rais Dk. Mwinyi wenye kuitekeleza vyema Ilani ya Uchaguzi ya chama cha Mapinduzi na kueleza kwamba muda wote wako tayari kushirikiana na Serikali pamojana kutekeleza maagizo ya ya Chama kwa lengo la kupiga hatua mbele kimaendeleo.

Walieleza imani yao kubwa kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Dk. Hussein Ali Mwinyi na kumuahidi mafanikio makubwa na ushindi wa kishindo mwaka 2025.Hata hivyo, walimueleza Rais Mwinyi dhamira yao njema ya kuweka vitega uchumi vyao kwenye eneo la maskani yao ambapo walisema wanatarajia kupata kipato cha kuiendesha maskan yao.

Maskani ya Kachorora ilizinduliwa Februari 03 mwaka 2011, wakati wa shamrashamra za maadhimisho ya kilele cha miaka 34 ya Chama Cha Mapinduzi na aliekua Makamu Mweyekiti kwa wakati huo, Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, awamu ya Sita Dk. Amani Abeid karume.