RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la   Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi amesema uamuzi wa kufanyika kwa Kongamano la Mahakama za Kikanda na Kitaifa Barani Afrika, utainufaisha sana Zanzibar na kuwawezesha Majaji na Viongozi mbali mbali wa kada ya sheria kushiriki na kuwaongezea maarifa na uzoefu.Dk. Mwinyi amesema hayo katika uzinduzi wa Kongamano la Mahakama za Kikanda na Kitaifa Barani Afrika lililofanyika katika Ukumbi wa Verde Mtoni Zanzibar.

Amesema Kongamano hilo ni muhimu kwa maendeleo na ufanisi wa mahakama pamoja na kada ya sheria nchini, jambo litakalowawezesha washiriki ikiwemo Majaji na wataalamu wengine wa Kada hiyo kupata maarifa na uzoefu, sambamba na kutanua wigo wa ushirikiano na wataalamu wengine kutoka nchi mbali mbali Barani Afrika.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimeweka kipaumbele katika utekelezaji wa masuala ya Haki za Binadamu kama zilivyobainishwa katika Katiba zao.

Aliyataja mambo kadhaa yanayolalamikiwa na kudhihirisha uvunjaji wa haki za Binadamu kwa jamii, kuwa ni pamoja na baadhi ya makundi kunyimwa haki za msingi, uonevu, ukatili, unyanyasaji na kutokuwepo uhuru katika masuala muhimu pamoja na ubaguzi wa aina mbali mbali.

“Tumeunda Tume ya Haki za Baindamu katika Utawala Bora inayoendelea kufanya akzi vizuri katika kuimarisha Haki za Bainadamu katika pande zote mbili za Muungano wetu”, alisema.

Aidha, alisema Serikali hizo zimekuwa zikishirikiana na Jmuiya mbali mbali za Kikanda na Kimataifa zinazoshughulikia masuala ya Haki za Binadamu Barani Afrika na Duniani kote.

Dk. Mwinyi alisema juhudi za pamoja za kuanda na kuendesha makongamano na mijadala ya aina hiyo ina umuhimu mkubwa   katika kujadili mafanikio na changamoto zinazoikabili kada hiyo katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo.

Alisema mikusanyiko ya aina hiyo ni muhimu katika juhudi za kujenga na kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kikazi miongoni mwa Majaji, wanasheria pamoja na taasisi zinazoshughulikia masuala ya kisheria.

Alisema mjadala juu ya suala hilo pia una umuhimu mkubwa kwa kuzingatia suala la Haki za Binadamu ni muhimu katika maisha ya binadamu, ikijumuisha mambo mbali mbali ambayo yameingizwa katika Katiba.

Nae, Nae Rais wa Mahakama ya Haki ay Afrika Mashariki Jaji Nestor Kayobera alisema Mahakama hiyo imeendelea kuitumia Mahakama iliopo Jijini Afrika kwa wastani wa kipindi cha maiak 20 sasa, pamoja na kuwa na Majaji sita.

Aidha,  Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu Jaji Iman Daud alisema maendeleo ya kijamii barani Afrika yatategemea zaidi namna viongozi wa Bara hilo watakavyojidhatiti katika kusimamia haki za binadamu katika mambo mbali mbali ikiwemo, ghasia zitokanazo na medani ya kisiasa.

Kongamano hilo la siku tatu linahusisha Mahakama tatu, ikiwemo Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu, Mahakama ya Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) pamoja na Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki, likifanikishwa kwa msaada wa wa Taasisi ya haki za Binadamu ya Raoul Wallenbergh kupitia msaada wa Shirika la Maendeleo la Sweeden, sambamba na ushirikiano wa Konrad Adenauer Stiftung, GIZ na Ofisi ya Tume ya Umoja wa Mataifa ya haki za Binadamu.

Kongamano hilo la siku tatu linahusisha Mahakama tatu, ikiwemo Mahakama ya Afrika ya haki za Binadamu, Mahakama ya Jumuiya Afrika Magharibi (ECOWAS) pamoja na Mahakama ya Jumuiya Afrika Mashariki.

Aidha washriiki wa Kongamano hilo ni pamoja na Majaj, Mawakili na watendaji mbali mbali wa sekta ya Mahakama Afrika.