Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amelipongeza Baraza la Mji Kati kwa kutekeleza kwa vitendo maagizo aliyoyatoa katika ziara yake ya mwaka jana na kueleza jinsi ya Mkoa wa Kusini ulivyomfurahisha kuliko mikoa yote aliyoitembelea katika ziara zake.Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo huko Dunga mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa soko la mbogamboga ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kutembelea miradi ya maendeleo hapa nchini.
Rais Dk. Mwinyi alisema kwamba katika ziara zake zote alizoitembelea mikoa ukiwemo Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkoa wa Kaskazini Unguja na ukubwa wa Halmashauri zao pamoja na Manispaa na Majiji lakini hawakumueleza chochote walichokifanya kinachotokana na makusanyo ya Halmashauri zao.“Katika ziara yangu niliyoaza Mkoa wa Mjini Magharibi pamoja na ukumbwa wao na kuwa Mjini, ukubwa wa Manispaa zao hawajanieleza chochote walichojenga”,alisema Dk. Mwinyi.
Mapema asubuhi akianza ziara yake mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika hospitali ya Wilaya ya Kati huko Mwera Pongwe, Rais Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kuipongeza Kampuni ya RANS kwa kufanya kazi ya ziada kutokana na changamoto ya ardhi katika eneo lililojengwa hospitali hiyo.Rais Dk. Mwinyi alisisitiza haja ya kuhakikisha huduma zitakazotolewa katika hospitali hizo mpya zinaendana na majengo hayo mapya yanayojengwa hapa nchini.
Mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji huko Mgenihaji, Rais Dk. Mwinyi aliwahakikishia wananchi wa Mgenihaji, Uzini pamoja na vitongoji vyake kwamba tatizo la maji litaondoka na litakuwa historia kutokana na juhudi kubwa zinazochukuliwa na Serikali anayoiongoza.Hivyo, Rais Dk. Mwinyi alisisitiza haja kwa Wizara kupitia Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), kuhakikisha miundombinu hya maji inatunzwa pamoja na watendaji kufanya kazi ipasavyo ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi huku akiitaka Mamlaka hiyo kuwaondoa wale wasiofanya kazi vyema.
Rais Dk. Mwinyi pia, alieleza hatua zinazochukuliwa katika kuhakikisha miradi inawanufaisha wananchi kwa kuweza kupata huduma za kijamii zikiwemo maji, afya, ajira pamoja na uwezeshaji wananchi kiuchumi.Alieleza hatua zinazoendelea kuchukuliwa katika kuhakikisha kilimo cha umwagiliaji maji kinaimarishwa hapa nchini na wakulima hasa wa mpunga wanavuna zaidi ya mara moja ndani ya mwaka.
Aliwaleza wananchi kwamba juhudi za makusudi zitaendelea kuchukuliwa na Wakandarasi ili kuhakikisha mnamo mwezi wa Disemba mwaka huu mradi huo unakamilika huku akieleza kwamba Serikali itahakikisha vipaumbele vyote vilivyowekwa na Jimbo hilo vinatekelezwa.Akiwa Jendele, Rais Dk. Mwinyi aliipongeza Wilaya hiyo kwa kupata bahati ya kujengewa skuli hiyo ya Elimu Mjumuisho ambapo skuli hiyo ipo moja tu kwa hapa Unguja na nyengie inajengwa huko Pujini Kisiwani Pemba.
Alisema kwamba skuli hiyo ni ya kwanza kutokana na mahitaji yake na umuhimu wake hapa nchini huku akisisitiza kwamba ni vyema wakawepo walimu maalum na wa kutosha kutokana na mahitaji maalum ya skuli hiyo.Pamoja na hayo, Rais Dk. Mwinyi aliwaeleza wananchi wa Ukongoroni na Charawe kwamba Serikali anayoiongoza itahakikisha inautekeleza ujenzi wa barabara katika vijiji hivyo pamoja na kupeleka huduma muhimu ya maji safi na salama.
Aliipongeza Wizara ya Elimu kwa kubuni mradi huo na kumpongeza Mkandarasi wa Kampuni ya Mwamba na unasoimamiwa na Kampuni ya “Edge Consultancy Company” ya haha hapa Tanzania aliyojenga skuli hiyo na kuwaongeza mwezi mmoja ili kuhakikisha wanakamilisha ipasavyo ujenzi huo.Pia, alieleza juhudi zitakazochukulwia na Serikali katika kuwawezesha wakulima na wavuvi ili waweze kufanya shughuli zao ipasavyo huku akiahidi Serikali kujenga viwanda viwanda vidogo vidogo kwa ajili ya kuwasaidia wakulima wakiwemo wakulima wa ndimu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Khamis alieleza kwamba kwa Zanzibar ni mara ya kwanza kujenga skuli hiyo ya Elimu Mjumuisho ambayo itatoa huduma kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum na wale wa kawaida katika eneo hilo.Alisema kuwa skuli hiyo ina madarasa manane, ofisi ya mwalimu mkuu, ofisi ya msaidizi mwalimu mkuu,vyoo10, ukumbi wa chakula, nyumba mbili za walimu zenye uwezo wa kukaa familia nne, kituo cha afya, Dakhalia mbili za wanafunzi zenye uwezo wa kukaa wanafunzi 160 kwa wakati mmoja.
Nao wananchi wa Jendele walieleza jinsi walivyofarajika kwa kuwepo skuli hiyo ya Mjumuisho na kueleza kwamba hatua hiyo itasaidia kukitangaza kijiji hicho kutokana na maendeleo yaliyofikiwa.
Nae Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Lela Mohammed Mussa aliitaka jamii kuhakikisha wanannchi hawawaweki majumbani watoto wenye mahitaji maalum na badala yake wazitumie skuli hiyo ipasavyo.Alisema kwamba skuli hizo ni za pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na tayari UNICEF imeonesha nia ya kupanua wigo kutokana na mradi huo na umuhimu wake katika jamii.
Nao viongozi wa Jimbo hilo walitoa pongezi kwa Rais Dk. Mwinyi kutokana na juhudi zake alizozionesha za kuwaunga mkono katika kuwapelekea maendeleo wananchi.
Mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika kituo cha wafanyabiashara huko Hanyenwga Mchana ambao ni mradi wa UVIKO -19, Rais Dk. Mwinyi alisema kwamba Serikali imechukua hatua ya kujenga miradi hiyo ili kuhakikisha Wajasiriamali wanapata nafasi ya kufanya shughuli zao.Alisema kwamba hatua ya ujenzi wa vituo kama hivyo itaendelezwa ili kuweza kuwasaidia Wajasiriamali huku akiahidi Serikali kutoa fedha wka ajili ya kukamisha eneo lililobakia ambalo tayari limeanza kujengwa huku akikipongeza kiksi cha Zima Moto na Uokozi kwa ujenzi mzuri wa kituo hicho.