RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema ufunguzi wa Chuo Kikuu cha Teknolojia cha India nchini ni utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya mwaka 2050.Alisema, chuo hicho cha Indian Institute of Technology Madrasa (IITM) ilikua ndoto yake ya kuifanya Zanzibar iendelee kutangazwa na kujulikana kimataifa na ujio wa chuo kikubwa na cha kwanza kwa ubora India hapa visiwani, umefanikisha ndoto yake na kuongeza kuwa chuo hicho ni miongoni mwa kazi zake zilizopata mafanikio makubwa kwa kipindi chake hiki cha Urais.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo kampasi ya Bweleo Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi alipozitundua rasmi chuo hicho.Alisema, lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kukifunguwa chuo hicho Unguja ni kuleta mabadiliko na maugezi makubwa ya maendeleo ya nchi na watu wake, kielimu, uchumi na jamii.Dk. Mwinyi, alieleza ili kuifikia Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inahitaji kuwekeza zaidi na kuwatayarisha wafanyakazi wenye utaalamu na ujuzi wa hali ya juu ili kujenga uchumi na jamii iliyo bora.

Alisema, Afrika ikiwemo Tanzania na Zanzibar kwa ujumla wanahitaji wataalamu wa teknolojia ili kusaidia kukabiliana na changamoto za maendeleo zinazowakabili, na kueleza ni matumaini ya Serikali kupata wataalamu waliojengewa maarifa na ujuzi unaohitajika duniani pia watatua changamoto zinazozikabili sekta mbalimbali zikiwemo nishati, kilimo, afya, elimu viwanda na nyengine.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi alitoa wito kwa vyuo vyengine nchini na Afrika kwa ujumla kutumia fursa ya kuwepo kwa chuo cha IIT Madrasa, Zanzibar kuanzisha ushirikiano ili kukuza uwezo na hadhi ya vyuo vyao na kueleza hadi sasa Chuo hicho tayari kimeingia makubaliano ya ushirikiano na vyuo vyengine vinne duniani, kikiwemo Chuo cha Uingereza cha Birmingham, Chuo cha Uchumi cha Afrika, chuo cha Daeakin cha Australia na chuo cha Teknolojia na Uongozi cha Nigeria.

Alisema chuo hicho ni fursa adhimu kwa wataalamu wa ndani kubadilishana uzoefu na waataalamu wa India hasa kwenye teknolojia, utafiti na Uvumbuzi.Naye, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Muhamed Mussa aliwahakikishia hali ya usalama, utulivu na amani, wageni, wahadhiri na wanafunzi wanaotoka nje ya Tanzania watakaosoma kampasi hiyo ya Bweleo.

Alisema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itajitahidi kukikuza chuo hicho kiwe bora zaidi duniani ili kuendelea kiitangaza Zanzibar kimataifa.Akizungumza kwenye ghafla hiyo, Balozi wa India nchini Tanzania, Binaya Pradhan alieleza kunzishwa kwa tawi la chuo cha IIT Madrasa hapa Zanzibar imekua ni sehemu ya mafanikio yake makubwa kuwahi kuyapata tokea kuanza kazi zake za Diplomasia hasa akiwa Balozi wa India Tanzania na kueleza anavijunia mafanikio hayo kwenye utumishi wake.

Mkurugenzi Mtendaji wa chuo hicho, Prof. Preeti Aghalayam alieleza matarajio ya chuo hicho ni kutoa wataalamu waliojengeka kitaaluma na uwezo wakujikimu kwenye ubobezi wa masuala teknolojia yatakayoleta mageuzi makubwa kwenye tehama na maendeleo ya uchumi wa mataifa yao.Jumla ya wanafunzi 46 wakiwemo Watanzania 21 kutoka bara na visiwani wamejiunga chuoni hapo na wengine kutoka maifa mengine ikiwemo Nepal.

IIT ni Chuo Kikuu chenye kujitegemea kinachotoa kozi mbalimbali za teknolojia, kuanzia Shahada ya kwanza, ya Pili na Shahada ya Udaktari (Ph.D) katika fani za teknolojia na sayansi, chuo hicho kinapokea wanafunzi kutoka Mataifa mbalimbali duniani.Ushirikiano baina India na Tanzania ni wahistoria,umeendelea kuimarika kwa fursa nyingi za maendeleo kupatikana kwa watu wa mataifa mawili hayo, Tanzania inaongoza kupata misaada wa nafasi nyingi za udhamini wa masomo nchini India kuliko nchi nyenyine yoyote barani Afrika, kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina yao.