RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameshukuru ushirikiano wa karibu uliopo baina ya Tanzania hususani Zanzibar, na Benki ya Dunia (WB), Umoja wa Ulaya (EU) na ushirikiano wa diplomasia uliopo baina ya Australia na Tanzania.Dk. Mwinyi alitoa shukurani hizo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na wageni hao walioambatana na ujumbe waliofuatana nao kwa nyakati tofauti.

Alisema, taasisi hizo zinamchango mkubwa wa maendeleo ya Zanzibar hasa kukuza sekta ya Afya nchini, Elimu, Utalii na Uchumi wa Buluu.Akizungumza na Balozi wa Australia nchini Tanzania, Mhe. Luke William aliefika kumuaga, Rais Dk. Mwinyi alishukuru ushirikino mkubwa uliopo baina ya Tanzanzia na nchi hiyo na kumueleza juu ya Zanzibar inavyonufaika na sekta ya uvuvi na mwani uliowaneemesha kinamama wengi na vijana kwani asilimia 90 ya wakulima wake ni kina mama.

Pia, Rais Dk. Mwinyi alimueleza balozi huyo azma ya kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Austalia na Zanzibar hasa kwenye masuala ya uwekezaji, biashara na utalii.
Vile vile Rais Dk. Mwinyi alizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa masuala ya Bahari na Uvuvi wa Umoja wa Ulaya (EU), Bi. Charlina Vitcheva alimueleza kuwa Zanzibar ni kisiwa kilichozungukwa na bahari ya Hindi, kinajivunia fursa nyingi zinazotokana na rasilimali bahari kwa kujikita zaidi kwenye uchumi wa Buluu na Utalii.

Alimueleza Mkurugenzi huyo, Uchumii wa Buluu ni sekta muhimu kwa uchumi wa Zanzibar na kuongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inafanya kila iwezavyo kunufaika na fursa zinazotokana na sekta hiyo kwa ajili ya uchumi na watu wake.Aidha, alimueleza mgeni huyo kuimarisha zaidi ushirikiano wao kwenye sekta hiyo, ili kujenga uweledi kwani idadi kubwa ya Wazanzibari wamejikita zaidi na masuala ya uvuvi na ajira zinazotona na bahari.

Rais dk. Mwinyi alisema, Serikali pia inawaungamkono wavuvi na wakulima wa mwani nchini kwani imewawezesha kwa mitaji na vifaa pamoja na kuiungamkono sekta ya Utalii.
Kwa upande wao wageni hao walemueleza Rais Dk. Mwinyi juu ya kuendelea kuiungamkono Zanzibar na Tanzania kwa ujumla hasa kwenye masuala ya kuendeleza ushirikiano wao wa diplomasia na kuona fusra za uwekezaji na uchumi zilizomo Tanzanzia vinanufaisha pande zote na ushirikiano wao.