Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuchukua hatua za Makusudi za kimkakati kuhakikisha inazipatia Ufumbuzi Changamoto zinazowakabili Watu Wenye Ulemavu hapa Nchini. Rais Dkt, Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 3 Disemba 2025 katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani yaliofanyika Ukumbi wa Dkt, Ali Muhammed Shein, Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja.

Dkt ,Mwinyi amefahamisha kuwa Serikali inaendelea kuzingatia Ushirikishi na Upatikanaji wa haki za Msingi za Watu wenye Ulemavu na kwamba hakuna Mtu mwenye Ulemavu atakaeachwa Nyuma katika Upatikanaji wa fursa za Kijamii ,Kisiasa, Uongozi na Uwezeshwaji. Aidha Rais Dķt, Mwinyi amelihakikishia Shirikisho na Jumuiya za Watu wenye Ulemavu na Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu Ushirikiano wa kwango cha juu kuzifanyia Tathimini Changamoto zinazowakabili Watu Wenye Ulemavu kwa lengo ka kuzipatia Ufumbuzi.

Akizungumzia siku ya Maadhimisho hayo yanayofanyika siku chache baada ya kukamilika kwa Uchaguzi Mkuu Dkt, Mwinyi amewapongeza Watu wenye Ulemavu kwa Kushiriki na kujitokeza kwa Wingi kutekeleza haki yao ya Kikatiba ya Kupiga Kura. Rais Dkt, Mwinyi ameeleza kuwa Serikali inazingatia kikamilifu Upatikanaji wa haki za Watu wenye Ulemavu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Ujenzii wa Majengo ya Afisi za Umma,  Hospitali ,Skuli ,Miundombinu na Barabara kwa kuzingata mahitaji ya Watu wenye Ulemavu .

Amefahmisha kuwa Kwa Kuzingatia Mahitaji hayo Serikali imejenga Skuli za Dakhalia za Wanafunzi wenye Ulemavu Mbili Katika Mkoa wa Kusini Unguja na Mkoa wa Kusini Pemba na   inakusudia kujenga Skuli nyenginea Tatu Maalum kwa Wanafunzi wenye Ulemavu katika mikoa mengine iliobakia kwa ajili ya Wanafunzi wenye Ulemavu. Aidha ameahidi kwa Serikali kutoa ruzuku kwa Jumuiya za Watu wenye Ulemavu ,Vifaa saidizi , Mafunzo na Mikopo isio na riba ili kuwawezesha Kiuchumi na kuweza kujisaidia na kujitegemea wenyewe.

Rais Dķt. Mwinyi amesema Kupitia Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu Serikali imeendelea kutoa Vifaa saidizi Bure kwa Watu wenye Ulemavu na kuihamasisha Jamii kuwasajili Watoto wote wenye Ulemavu katika Jumuiya zao ili kuhakikisha wanapata Vifaa Saidizi bure. Amewahakikishia Watu wenye Ulemavu kuwa Serikali itaendelea kutoa MIkopo isio na Riba kutoka Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Fedha za Uwiano kutoka Serikali za Mitaa na Fursa katika Vyombo vya Maamuzi ili Kuliimarissha Kundi hilo.

Rais Dkt, Mwinyi amewashukuru Wadau wote wa Ndani na Wale wa kimataifa kwa kuendelea kuungana na Serikali kuwasaidia Watu wenye Ulemavu na kuzipatia Ufumbuzi Changamoto. Zinazowakabili.

Naye Kaimu Waziri wa Nchi,Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Hamza Hassan Juma amesema hatua ya Serikali ya kutoa Mikopo kwa Watu wenye Ulemavu kupitia Mtu mmoja mmoja ni hatua muhimu inayoacha Alama ya Uongozi wa Awamu ya Nane itakayowasaidia kujitegemea wenyewe. Maadhimisho ya Mwaka yamefanyika chini ya Kaulimbiu inayosema “Kukuza Jamii Jumuishi Kwa Watu Wenye Ulemavu ili Kuendeleza Maendekeo ya Kijamii Zanzibar.”