Mke wa Rais wa Zanzibar ambaye Pia Mwenyekiti na Msarifu wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama Mariam Mwinyi amesema Mapambano ya Ukatili wa Kijinsia Unaofanyika Mitandaoni Unahitaji nguvu ya pamoja na Ushirikiano wa Wadau ili kuutokomeza.
Mama Mariamu Mwinyi ameyasema hayo alipofungua Kongamano la Maadhimisho ya siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia lililofanyika Ukumbi wa Ali Muhammed Shein, Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja ambalo limeandaliwa na Jumuiya ya Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA).
Amefahamisha kuwa dhana ya Ukatili wa Kijinsia Umechukua Sura mpya kwa kufanyika zaidi Mitandaoni ambao umekuwa na athari kubwa zaidi ikiwemo Vitisho,Matusi ,na Kuchafuliana Majina .
Mama Mariam ameeleza kuwa Ukatili huo umekuwa una Athari kubwa kwa Waathirika kwani kunasababisha Unyanyapaa, Sonono na kufikia kujitoa Muhanga kwa Waathirika .
Mwenyekiti huyo wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation amesema Umefika wakati wa kuwa na nguvu ya Pamoja ili Kuutokomeza hususani ukatili unaofanyika Mitandaoni kwa Kuangalia Upya Mifumo ,Mitazamo na mienendo inayoruhusu ukatili kuendelea .
Aidha amesema Ukatili huo sio tatizo la mtu mmoja mmoja bali ni Changamotio ya Kijamii inayohitaji Ushirikiano ,Hatua Thabit na Uongozi madhubuti .
Amefahamisha kuwa Tatizo hilo haliwezi kutatuliwa na Mtu Bali ni lazima Taasisi kuungana pamoja na Serikali, Asasi za Kiraia ,Taasisi za Kidini na Watoa huduma za Mitandaoni ili kulitokomeza Kabisa.
Akizungumzia juhudi na Mikakati inayochukuliwa Na Taasisi yake ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama Mariam Mwinyi amesema imeendelea kuungana na Taasisi na Wadau wote kutokomeza Ukatili wa Kijinsia Mitandaon.
Amesema Tayari ZMBF kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia , Wazee na Watoto wanatengeneza Mfumo wa Kidigitali unaolenga Utoaji wa Taarifa za Ukatili wa Kijinsia ,Utunzaji wa Kumbukumbu na Ufuatiliaji wa Matukio ya Ukatilli na Unyanyasaji wa kijinsia katika ngazi zote.
Mfumo huo wa Zanzibar GBV Case Information and Management System unaolenga kuimarisha Uratibu ,Uwajibikaji , Upatikanaji wa Huduma kwa Waathirika kwa Ufanisi zaidi .
Aidha amesema ZMBF katika kuunga mkono juhudi za Serikali Taasis hiyo imeendelea kutoa huduma mbalimbali kwa Wanufaika 3,667 ikiwa ni pamoja na kuwapatia Elimu ya kujikinga na Udhallilishaji,Kuwaunganisha Waathirika na Huduma za Afya ,Ushauri nasaha pamoja na Huduma za Msaada wa huduma za kisheria kupitia kambi za Afya Bora - Maisha Bora.
Mama Mariamu Mwinyi amewasisitiza Washiriki wa Kongamano hilo wakiwemo Majaji na Mahakimu Wanawake Kujitathimini na kuhamasisha na kuja na mikakati itakoyosaidia kuchukua hatua madhubuti za kukomesha Ukatiili wa Kijinsia hususan wa Mitandaoni.
Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe,Anna Athanas Paul ameisisitiza TAWJA kuweka Mkazo zaidi kuhakikisha Upatikanaji wa Haki za Waathirika wa Ukatili wa kijinsia katika Vyombo vya Sheria na kuwataka kufanya kazi kwa Ushirikiano kufikia Malengo.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) Jaji Aziza Iddi Suweid amesema Jumuiya hiyo imejipanga kukuza na kuendeleza Upatikanaji wa Haki kwa Usawa na kuuelimisha Umma juu ya Kutathimini Upatikanaji wa haki katika nyanja zote za kisheria katika jamii .
