Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam H. Mwinyi, ambaye pia ni Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), ameendelea kuonesha uongozi thabiti katika kampeni y
Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam H. Mwinyi, ambaye pia ni Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), ameendelea kuonesha uongozi thabiti katika kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia. Kampeni hii inalenga kuongeza uelewa wa jamii kuhusu athari za ukatili wa kijinsia, njia za kujilinda, na umuhimu wa kuchukua hatua za pamoja kukomesha tatizo hili.