RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Mwinyi amejumuika na waumin mbali mbali katika Ibada ya Sala ya Ijumaa iliofanyika Msikiti wa Ijumaa Miembeni, Mkoa Mjini Magharibi.
Mapema, akisoma hotuba ya Sala hiyo ya Ijumaa, Khatibu wa Msikiti huo Sheikh Khalid Ali Mfaume, aliwataka waumini kutumia vyema siku kumi za mwanzo wa Mwezi huu wa Mfunguo tatu (Dhulhijjah) kwa kudumisha ibada kwa ajili ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu.
Akielezea miongoni mwa Ibada hizo, Sheikh Khalid ambae pia ni katibu Mtendaji ofisi ya Mufti wa Zanzibar alizitaja kuwa ni pamoja na kuchinja kuambatana na sifa na aina za wanyama wanaofaa kuchinjwa, wakati wa kuchinja na namna ya ugawaji wa kile kilichochinjwa.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa waumini kuendeleza malezi bora yatakayowafanya wazazi kuwa na ukaribu na watoto wao, hali inayojenga urafiki na akatolea mfano wa kisa cha Nabii Ibrahim (AS) na mwanawe Nabii Ismail (AS).
Wakati huo huo, Alhaj Dk. Mwnyi alipata fursa ya kufika nyumbani kwa Mbunge wa Jimbo la Bububu (CCM) Bi Mwantakaje Haji Juma kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kufuatia kufiwa na mumewe pamoja na kufika Dole Ndunduke kutoa mkono wa pole kwa Mfanyakazi wa Ofisi yake kutokana kifo cha Baba yake mzazi Marehemu Hamdoun Suleiman Soraga