Rais wa Zanzibar Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi ameshiriki kisomo cha Hitma na kutowa Mkono wa pole kwa Familia ya Marehemu Mussa Hassan Mussa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Amani Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akishiriki katika kisomo cha Hitma na Dua ya kumuombea Marehemu Mussa Hassan Mussa, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Amani Zanzibar, kisomo hicho kilichofanyika katika Msikiti wa Bwejuu Wilaya ya Kusini Unguja.