RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Kiongozi wa Jumuiya ya Istiqaama Zanzibar Sheikh.Sultan Khamis Mbarouk akizungumzia changamoto za Jumuiya yao wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 4-6-2022, walipofika kujitambulisha na kuelezea kazi za Jumuiya yao kwa Jamii ya Zanzibar.