RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi leo amewapisha watendaji mbali mbali wa Wizara za Serikali aliowateuwa hivi karibuni kushika nyadhifa zao .
Katika hafla iliofanyika Ikulu Zanzibar na kuhudhuriwa an Viongozi mbali mbali wa kitaifa, akiwemo Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla, Dk. Mwinyi amemuapisha Dk. Islam Seif Salum kuwa Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais pamoja na Maryam Juma A. Sadalla kuwa Katibu Mkuu (Kazi na Uwezeshaji) katika Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji.
Aidha, alimuapisha Abeda Rashid Abdalla kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto.
Katika hatua nyengine, Dk. Mwinyi alimuapisha Saleh Juma Mussa kuwa Katibu Mkuu (OR) Ikulu, Khamis Abdalla Said kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, sambamba na Thabit Idarous Faina aliemuapisha kushika wadhifa wa Mkurugenzi wa uchaguzi katikaTume ya Uchaguzi.