Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mwinyi amefungua Mafunzo ya Awali kwa Viongozi Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, yaliyofanyika katika Chuo cha IIT Madras, Bweleo,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mwinyi amefungua Mafunzo ya Awali kwa Viongozi Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, yaliyofanyika katika Chuo cha IIT Madras, Bweleo, Mkoa wa Mjini Magharibi.Katika hotuba yake, Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza kwamba mafunzo hayo yana lengo la kuimarisha usimamizi bora wa utendaji, kuongeza uwajibikaji, na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.