Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameongoza Kikao cha kwanza cha Baraza la Mapinduzi (BLM).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameongoza Kikao cha kwanza cha Baraza la Mapinduzi (BLM) katika kipindi cha pili cha Serikali ya Awamu ya Nane. Katika kikao hicho, kilichofanyika Ukumbi wa Baraza la Mapinduzi, Rais Dkt. Mwinyi pia ameongoza hafla ya uapisho wa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mhe. Mgeni Khatibu Yahya, aliyeteuliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo.