Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, pamoja na Mkewe Mama Mariyam Mwinyi wakishiriki katika Bonanza la 16 la Mazoezi ya Viungo lililoandaliwa na Chama c
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, pamoja na Mkewe Mama Mariyam Mwinyi wakishiriki katika Bonanza la 16 la Mazoezi ya Viungo lililoandaliwa na Chama cha Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA), lililofanyika katika Uwanja wa New Amaan Complex, Mkoa wa Mjini Magharibi. Bonanza hilo limehusisha vikundi 165 vya mazoezi kutoka vilabu 25 vya Pemba, 100 vya Unguja na 40 kutoka Tanzania Bara, likiwa na washiriki zaidi ya 500.