SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inajitahidi kuboresha mazingira wezeshi kwa watu wenyeulemavu kwenye sekta zote za jamii zikiwemo Usafiri wa umma, Elimu na Afya kwa kuzingatia na kurahisisha mahitaji yao.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na ujumbe kutoka Shirika la kimataifa la Christian Blind Mission (CBM) waliofika kumtembelea.Alieleza kufurahishwa kwake na ushirikiano uliopo baina ya Serikali na Shirika hilo kupitia Wizara ya Afya Zanzibar.

Dk. Mwinyi amesema Serikali ikiwa kwenye mchakato wa kutoa huduma za Bima ya afya kwa wananchi wa Unguja na Pemba, kipaumbele zaidi kimezingatiwa kwa watu wenyeulemavu, Zanzibar.Akizungumzia sera ya watu wenyeulemavu ya Zanznibar, Rais Dk. Mwinyi alieleza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatekeleza sera hiyo kwa vitendo kwa kuzingatia matakwa na mahitaji ya jamii hiyo hata kwenye majengo yote ya umma inaweka mkazo zaidi kwa mahitaji yao ikiwemo kuboresha miundombinu ya majengo na ofisi za Serikali kufikiwa na watu wajamii zote ikiwemo huduma za ngazi na vyoo kuwa na mazingira rafiki kwa watu wote.

Akizungmzia mpango mpya wa huduma za usafiri wa Umma ambao Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeadhimia kuboresha huduma hiyo kwa jamii, Rais Dk. Mwinyi pia alieleza Serikali imewazingatia watu wenyeulemavu na kuangalia uwezekano mkubwa wa kuwafikia kwenye huduma wezeshi za usafiri huo huku akieleza wadau zaidi wanahitajika kuunga mkono kwenye sekta ya afya kwa watu wenyeulemavu.“Kwenye sekta ya elimu wadau wengi wamejitoleza kuungamkono sekta hiyo, mchango zaidi unahitajika kwenye sekta ya Afya” Alifafanua Dk. Mwinyi.

Aidha, aliiomba taasisi ya CBM, kuangalia uwezekano wa kuungamkono suala Makaazi kwaajili ya watu wenyeulemavu, kwani Serikali ina nia ya kuboresha huduma hiyo, pamoja na kuwakaribisha wadau wengine wa maendeleo kuungamkono huduma hiyo kwa Serikali.Nesia Satoki Mahenge, Mkurugenzi Mkaazi wa CBM, Tanzania alimueleza Rais Dk. Mwinyi kwamba taasisi yao inashirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya, kwenye Hospitali ya rufaa ya Mnazi Mmoja.

Alieleza, CBM inashirikana na hospitali ya Mnanzi Mmoja kutekeleza mradi wa kusimamia na hutoa huduma za matibabu kwa watu wenyeulemavu ambapo imetoa kiasi cha shilingi bilioni moja kwaajili ya kuisadia hospitali hiyo kutoa huduma za afya ya macho, kuwasaidia watu wenye ulemavu kupata huduma na matibabu ya macho, kununulia dawa, vifaa vya kutoa huduma kwa watu wenye ulemavu, kununulia vitendea kazi, kuboresha miundombinu ya hospitali kuwa rafiki kwa wenyeulemavu, pamoja na gharama za kuzifikia jamii ili kubaini matatizo ya watu wenyeulemavu yanayowakabili kiafya na kutoa vifaa kwaaajili ya kuwasaidia watoto wenyeulemavu wa macho.

Naye, Mkurugenzi Maendeleo Jumuishi CBM, Dominique Schlupkothen alimueleza Dk. Mwinyi kwamba taasisi hiyo inafanyakazi kwa ushirikiano mkubwa na Serikali, taasisi binafsi pamoja na wadau wengine wa maendeleo, mbali na kujikita kwenye kutoa huduma za afya ya macho pia wamejikita na miradi inayoshughulikia maradhi yasiyopewa kipaumbele duniani yakiwemo mabusha, minyoo na maradhi mengine.CBM ni taasisi isiyo ya serikali inafanyakazi kwenye maeneo ya kuwasaidia watu wenyeulemavu kwa nchi 44 duniani, kwa ushirikiano wa Serikali na taasisi binafsi kwa Tanzania ikiwemo Zanzibar. 

Ujumbe wa CBM Ikulu, uliongozwa na Waziri wa Afya, Ahmeid Mazrui, awali walifanikiwa kutembelea skuli ya msingi ya elimu jumishi, Kisiwandui