Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar inajipanga kuendelea kujenga Miundombinu ya Viwanja vya Ndege ili kuiifanya kuwa Kituo bora cha Utoaji wa huduma za Usafiri wa Anga. Dkt, Mwinyi ametoa tamko hilo alipofungua Mkutano wa Huduma za Usafri wa Anga pamoja na Utalii Afrika katika Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege. 

Ameeleza kuwa Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume na Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba ni Miongoni mwa juhudi zinazochukuliwa na Serikali za kuimarisha huduma za Usafiri wa Anga hapa Nchini.Dkt, Mwinyi amefahamisha kuwa hatua hiyo itaifungua Zanzibar Kikanda na Kimataifa kwa Mashirika zaidi ya Ndege kuja Nchini na kuongeza Idadi ya Watalii wanaokuja nchini pamoja na kuutangaza Utalii . 

Aidha amesema huduma za Usafiri wa Anga ni Kichocheo muhimu cha Ukuaji wa sekta ya Utalii inayochangia asilimia 30 ya pato la Nchi Kiuchumi na ni uti wa Mgongo wa Uchumi wa Zanzibar.Rais Dkt, Mwinyi ameeleza kuwa katika Miaka ya Karibuni kumeshuhudiwa Ukuaji Mkubwa wa Sekta ya Utalii kulikochangia na Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Filamu ya Royal Tour ilioitangaza Tanzania ikiwemo Zanzibar na kutambulika kwa vivutio vya Utalii, Utamaduni na Urithi wa Kihistoria.

Aidha amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha huduma katika Viwanja vya Ndege ikiwemo kushirikina na Sekta binafsi kupitia Sera ya PPP, Mashirika ya Ndege ya Kikanda na Kimataifa na kusimamia ipasavyo Kanuni na Miongozo ya Huduma za Usafiri wa Anga na hali ya Usalama wa Nchi hatua inayochangia Kuongezeka kwa Mashirika ya Ndege yanayaotoa huduma Nchini.

Rais Dkt, Mwinyi amewasisiriza Washiriki wa Mkutano huo kufanya kazi kwa pamoja na kuunga mkono juhudi za Zanzibar zenye lengo la kuifanya kuwa Kituo bora cha Huduma za Usafiri wa Anga Kimataifa.Mkutano huo wa Kimataifa wa Masuala ya Anga na Utalii ni wa Tisa kufanyika na ni wa Siku tatu ambapo umeyajumuisha Mashirika takribani 40 ya Ndege Barani Afrika.