Katika salamu hizo Dk. Shein alieleza kuwa wananchi wa Zanzibar wanaungana pamoja na ndugu zao wa Uturuki katika kusherehekea siku hii adhimu na muhimu katika historia ya nchi hiyo.

Aidha, salamu hizo,zilieleza kuwa tukio hilo kubwa, linatoa nafasi ya kuendeleza uhusiano na ushirikiano mkubwa kati ya Jamhuri ya Watu wa Uturuki na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Sambamba na hayo, Dk. Shein alimtakia kiongozi huyo pamoja na familia yake na wananchi wote wa Jamhuri ya Uturuki afya na sherehe njema katika kuadhimisha siku hiyo huku akimtakia kiongozi huyo mafanikio zaidi katika kuendelea kuipatia
maendeleo zaidi ya kiuchumi nchi hiyo kwa madhumuni ya kulinufaisha Taifa hilo pamoja na watu wake.

Jamhuri ya Uturuki ilianzishwa mwaka 1923 na Jenerali Kemal Ataturk ambayo iliundwa na kuwa Taifa baada ya vita vikuu vya Kwanza vya dunia ambapo kabla ya hapo Waturuki walikuwa chini ya milki ya Osmani (Ottoman Empare)
iliyounganisha mataifa mengi ya Sultan wa Konstantinopoli wakati huo