Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduz iMhe,Dkt Hussein Ali Mwinyi amekutana na Katibu Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman, Bw Jamal Moussa Al - Moosawi   kwa Mazungumzo maalum katika Muendelezo wa kuimarisha Uhusiano na Ushirikiano katika Maeneo ya Uendelezaji na Uhifadhi wa Maeneo ya Urith wa Kihistoria na Utamaduni wa Zanzibar

Mazungumzo hayo Yamefanyika leo tarehe 5 Agosti 2026 Ikulu, Zanzibar ambapo Pia yalihudhuriwa na Balozi Mdogo wa Oman aliopo Zanzibar Mhe ,Said Salim Al Sinawiy .

Rais Dkt, Mwinyi amepongeza juhudi za Serikali ya Oman za kuendeleza Misaada na Ushirikiiano wa dhati kuhakikisha Zanzibar inafanikiwa katika kuimarisha Uhifadhi wa Urithi wa Kihistoria na Utamaduni wake kwa kuendelea kuunga Mkono Mipango   na Miradi mbalimbali ya Uhifadhi,Uendeshaji na Uendelezaji wa Maeneo muhimu ya Kumbukumbu za Urithi wa Kihistoria na Utamaduni wa Zanzibar aliyoielezea kuwa ni hatua yenye Umuhimu Mkubwa kwa Uchumi na Maendeleo ya Zanzibar.

Rais Dķt Mwinyi ameihakikishia Oman Ushirikiano mkubwa katika kufanikisha programu na Uendelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Oman hapa Zanzibar hususani katika Uhifadhi wa Urithi wa Kihistoria na Utamaduni.

Ameiomba Oman kuendeleza Programu za Mafunzo ya kujenga Uwezo kwa Wataalamu wa ndani na kuwapatia Mbinu na Teknolojia za kisasa katika kuimarisha Uhifadhi wa Urithi wa Maeneo ya Kihistoria na Usimamizi na Uendeshaji wa Kisasa pamoja na uhifadhi wa Kumbukumbu.

Naye Katibu Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman ,Bw, Jammal Moussa Al Moonsawi ameihakikishia Zanzibar kuwa Nchi hiyo itaendelea kushirikiana nayo katika kuimarisha Maendeleo ya Uhifadhi wa Urithi wa Kihistoria na Kumbukumbu muhimu za Kisiasa, Utamaduni na kijamii ziliopo Zanzibar ikiwa ni hatua muhimu ya kuimarisha Uhusiano na Ushirikiano wa muda mrefu wa Zanzibar na Oman .