Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewaapisha viongozi wanne aliowateua hivi karibuni, wakiwemo majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Rais Dkt. Mwinyi amewaapisha viongozi hao leo, tarehe 24 Julai 2026, katika hafla iliyofanyika Ikulu Zanzibar.
Viongozi waliokula kiapo ni:
1. Dkt. Mahadhi Juma Maalim
Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar.
2. Mhe. Valentina Andrew Katema
Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
3. Mhe. Khamis Ali Simai
Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
4. Dkt. Josephine Rogate Kimaro
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla; Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla; Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mhe. Zuberi Ali Maulid; Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Ndg. Mansoura Mossi Kassim; pamoja na Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Dini na wageni waalikwa.
.jpeg)