Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali inaendelea kutafuta vyanzo vipya na nafuu vya fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati na kuharakisha maendeleo ya Zanzibar. Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo leo, tarehe 10 Agosti 2026, alipokutana na Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Trade and Development Bank (TDB), Bw. Admassu Tadesse, pamoja na ujumbe wake Ikulu Zanzibar.
Amesema Zanzibar inalenga kutumia mifumo mbalimbali ya kifedha ili kuongeza fursa za uwekezaji katika miradi muhimu ikiwemo Bandari Jumuishi ya Mangapwani, nishati, makaazi, mafuta na gesi, pamoja na miradi ya maendeā¦
[12:33, 8/10/2026] Denis Bilal: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar inaendelea kutafuta vyanzo vipya na vyenye unafuu vya fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati na kuongeza kasi ya maendeleo, bila kutegemea mikopo ya kawaida na dhamana za Serikali pekee.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 10 Agosti 2026, alipokutana na Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Trade and Development Bank (TDB), Bw. Admassu Tadesse, na ujumbe wake katika mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Zanzibar.
Rais Dkt. Mwinyi amesema mifumo hiyo inaweza kufungua fursa mpya kwa Zanzibar katika kupata fedha za maendeleo, hususan kwa kuzingatia changamoto zinazoweza kujitokeza katika upatikanaji wa dhamana za Serikali kwa baadhi ya miradi. Amesisitiza umuhimu wa kuangalia vyanzo mbalimbali vya fedha vinavyoendana na mahitaji na vipaumbele vya maendeleo ya Zanzibar.
Akizungumzia maeneo ya uwekezaji, Rais Dkt. Mwinyi ametaja Bandari Jumuishi ya Mangapwani kuwa miongoni mwa miradi yenye fursa kubwa, kutokana na dhamira ya Serikali ya kuiendeleza kuwa bandari ya kupitishia mizigo kwenda maeneo mengine (Transshipment Port), pamoja na kuwa na huduma mbalimbali zikiwemo bandari kavu, mafuta na gesi, pamoja na uhifadhi wa nafaka.
Aidha, amesema sekta ya nishati ni eneo muhimu linalohitaji uwekezaji zaidi, hususan katika kuongeza uzalishaji wa umeme na uwezo wa Zanzibar kujitegemea kwa nishati kupitia vyanzo vya nishati mbadala. Amesema hatua hiyo ni muhimu katika kuimarisha uhakika wa nishati na kukidhi mahitaji yanayoongezeka kutokana na miradi mipya ya maendeleo na uwekezaji.
Rais Dkt. Mwinyi pia ameeleza fursa zilizopo katika sekta ya makaazi, akibainisha mpango wa Serikali wa kuongeza upatikanaji wa makaazi bora, ikiwemo pendekezo la ujenzi wa nyumba 10,000, pamoja na kuangalia mifumo ya fedha itakayowezesha Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC) kupanua utekelezaji wa miradi ya makaazi.
Ameeleza kuwa mafuta na gesi, uwekezaji kupitia mfuko ya hifadhi ya jamii, tafiti yakinifu pamoja na kuimarisha taasisi za fedha za ndani ni miongoni mwa maeneo yanayoweza kupewa kipaumbele katika kupanua fursa za uwekezaji na upatikanaji wa fedha.
Rais Dkt. Mwinyi ameueleza ujumbe huo kuwa Zanzibar pia iko tayari kuangalia fursa za kupata wawekezaji kupitia mtandao wa TDB katika miradi yenye tija na umuhimu wa kimkakati kwa maendeleo ya nchi.
Naye, Bw. Admassu Tadesse amesema TDB ina mifumo mbalimbali ya kifedha inayoweza kukidhi mahitaji ya miradi katika hatua mbalimbali, ikiwemo fedha za maandalizi ya miradi, mitaji yenye masharti nafuu, uwekezaji kupitia Sekta Binafsi na mifuko maalum ya uwekezaji. Aidha, ameihakikishia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ushirikiano wa karibu katika kufanikisha maeneo yatakayokubaliwa na pande hizo mbili.
