Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewataka wananchi kuendelea kulinda amani na utulivu, akisisitiza kuwa ni msingi muhimu wa maendeleo, uwekezaji, biashara na utalii nchini.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 09 Novemba 2026, katika Dua Maalumu ya Kitaifa ya kuiombea nchi amani na ulinzi dhidi ya majanga mbalimbali, iliyofanyika katika Msikiti wa Muembe Shauri, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Aidha, amewataka viongozi wa dini kuendelea kuhamasisha umoja, mshikamano na kuheshimiana, huku akisisitiza wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua za Vuli na El NiƱo.
Dua hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, pamoja na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein.
