Rais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Mwinyi ameweka Jiwe la msingi mradi wa Skuli ya Msingi Donge akiwa katika ziara yake Mkoa wa Kaskazini Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi mbalimbali zilizotolewa na Wananchi wa Donge kwa ajili yake, akikabidhi na Bi. Fatma Saleh (Bi.Ukindu) baada ya kuzungumza na Wananchi wa Kijiji hicho na kuweka Jiwe la Msingi la Skuli ya Msingi Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja,wakati wa ziara yake leo 23-10-2023