Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kutekeleza Miradi Mikubwa ya Kimkakati ya Maendeleo kwa lengo la kuijenga Nchi na kuandaa Maisha Bora kwa Wananchi.
Ameyasema hayo leo Tarehe 16 Mei 2026 alipokutana na Baraza Kuu la Wazee wa Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar katika Mkutano Maalum wa Kutoa Shukrani baada ya Kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2025 Hafla iliyofanyika Ikulu, Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti Dķt, Hussein ameeleza kuwa Kazi muhimu iliyobakia ni kuyatekeleza kwa Vitendo Mambo yote yaliyoainishwa katika Ilania ya Chama Cha Mapinduzi ili yawe yamekamilika ifikapo mwaka 2030.
Akizungumzia Miradi inayoendelea ya Ujenzi amesema Nia ya Serikali ni kujenga Nyumba za kisasa kwa ajili ya Makaazi ya Wananchi na kuwaondoa katika Majengo Chakavu yaliotumika kwa zaidi ya Miaka 60 ambayo yamekuwa sio salama tena.
AIdha ameeleza dhamira ya Serikali ya kuendelea Miradi zaidi katika sekta mbalimbali za Kiuchumi na kijamii ikwemo Sekta ya Afya,Elimu ,Miundombinu, Mawasiliano ,Bandari ,Barabara na Viwanja vya Ndege na Nuymba za Maendeleo za kisasa
Akizungumzia Suala la Serikali ya Umoja wa Kitaifa Makamu Mwenyekiti Dķt, Mwinyi amesema Majadiliano na Chama Cha ACT-WAZALENDO yanaendelea vizuri na Chama Cha Mapinduzi kinazingatia Maslahi ya Chama hicho na Taifa kwa Ujumla na kubainisha kuwa lengo kuu ni kuwa na Nchi Tulivu yenye Amani ,Umoja na Kuondoa Chuki miongoni mwa Wananchi.
Akiwasilisha Salamu za Wazee,Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi, Zanzibar Nd, Waziri Mbwana Ali amesema Baraza hilo limempongeza Makamu Mwenyekiti Dķt Mwinyi, kwa kuimarisha Umoja na Utulivu wa Nchi pamoja na Kuleta Maendeleo Makubwa katika Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara,Viwanja vya Ndege na dhamira ya Kimkakati ya kuifungua Pemba Kiuchumi sambamba na kuendeleza Majadiliano ya Kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kuahidi kumuunga mkono.
