Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali zote Mbili za SMZ na SMT zitaendeleza na kuweka   Mkazo maalum wa kumaliza Changamoto za Muungano ambazo bado hazijapatiwa Ufumbuzi. Amesema Serikali zitaendelea kuendeleza Vikao na Majadiliano kwa lengo la kuzipatia Ufumbuzi Changamoto ambazo bado ni Kikwazo kwa Muungano aliouelezea kuwa wa kipekee Duniani.

Makamu Mwenyekiti Dķt, Hussein Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 26 Aprili 2026 katika kongamano la kuadhmisha Miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililoandaliiwa na Umoja wa Vijana (UVCCM ) lililofanyika katika Chuo cha Vijana Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja. Kongamano lililofunguliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt, Samia Suluhu Hassan pamoja na kufunga Mafunzo ya Uongozi na Uzalendo kwa Makatibu na Wasaidizi Makatibu wa UVCCM.

Amefahamisha kuwa Miaka 62 ya Muungano imekuwa na Mafanikio.makubwa kwa pande zote mbili za Muungano Kisiasa, Kijamii na Kiuchumi na kuwasisitiza Watanzania kuuenzi na kuudumisha Muungano kwa manufaa ya Taifa la Tanzania. Makamu Mwenyekiti Dkt Hussein Mwinyi amempongeza Mwenyekiti wa Cha Mapinduzi Taifa Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa Utayari wake wa kuendeleza Dhamira na Malengo ya Muungano kama ulivoasisiwa na Waasisi wake Hayat Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume Mwaka 1964 na kuendelezwa na Viongozi wa Awamu zote zilizofuata.

Dkt, Mwinyi amewahimiza Watanzania hususani Vijana kuona Umuhimu wa kuilinda Amani na kuepuka Vishawishi vya Uvunjifu wa Amani na kuudumisha   Muungano kwani ni ngao muhimu ya Umoja , Mshikamano na Udugu pamoja na kuimarisha Amani na Utulivu wa Nchi na kuwahakikishia kuwa Serikali zote mbili zitaendelea kuendeleza juhudi mbalimbali za kumaliza Changamoto zinazowakabili Vijana hapa nchini .

Ameeleza kuwa Serikali zote mbili chini ya Usimamizii wa Chama Cha Mapinduzi Zimeunda Wizara maalum na zimeweka Mazingatio makubwa na kuzifanyia kazi changmoto mbalimbali zinazowakabili Vijana na kutenga Fedha maalum kwa Ajili ya kuwawezesha Vijana kupitia fursa mbalimbali ziliopo hapa Nchini ikiwemo fursa za Ajira ,nafasi za Uongozi   pamoja na ,kuboresha Mitaala ya Elimu ili Vijana waweze kuajirika au kujiajiri wenyewe kwa kuona Umuhimu wa kundi hilo kubwa la Vijana.

Akihitimisha hutuba yake Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt, Hussein Mwinyi ametoa wto kwa Vijana kuendelea kutumia fursa ziliopo kisiasa, kijamii na kiuchumi pamoja na kuwahakikishia Vijana kutekeleza Mambo yote aliyowaahidi wakati wa Kampeni za Uchaguzi. Dkt ,Mwinyi ameupongeza Umoja wa Vijana wa CCM kw kuona Umuhimu wa kuandaa Kongamano hilo la Miaka 62 ya Muungano wakati huu kukiwa na Mafanikio na Maendeleo makubwa ya Kisiasa ,kijami na Kiuchumi na Nchi ikiwa katika Amani na Utulivu.

Mwenyekiti wa CCM, Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Kongamano hilo la Kuadhimisha Miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar amewasisitiza Vijana kuimarisha Mshikamano kwani ndio nguzo muhimu ya Kuimarika Muungano , Umoja na Amani ya Taifa.