RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi leo amemuapisha Ali Khamis Juma kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Biashara , Viwanda na Masoko katika hafla iliofanyika Ikulu Zanzibar.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kabla ya uteuzi huo, Ali Khamis Juma alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.