Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk ,Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar Inaendelea Kuweka Mazingira Mazuri zaidi ya Kuwavutia Wawekezaji zaidi Kuwekeza nchini.Rais Dk, Mwinyi ametoa tamko hilo alipozungumza na Balozi wa Tanzania Nchini.Nigeria Balozi Celestine Kakele aliefika Ikulu Kujitambulisha.

Rais Dk, Mwinyi ameeleza kuwa kuna fursa kubwa ya Nchi hizo mbili kushirikiana hasa katika Sekta ya Utalii na Uwekezaji ambazo zikifanyika vyema nchi hizo zinaweza kunufaika kwa kiasi kikubwa.Dk,Mwinyi amemsisitiza Balozi Kakele kufanya juhudi Maalum za kuwavutia Wawekezaji kutoka Nigeria kuja Nchini kuangalia Fursa za Uwekezaji na Serikali inaanda Mazingira mazuri ya kuwa na Uwekezaji wenye tija na Endelevu.

Amemuhakikishia Balozi huyo kuwa Serikali inaimarisha Uwekezaji kwa Kuondoa Vikwazo vinavyozorotesha Ushirikiano kwa lengo la Kuwavutia Wawekezaji.Amefahamisha Kuwa Utalii na Uwekezaji ni Vichocheo Muhimu vya Uchumi wa Zanzibar hivyo ni vema akaweka Mkazo katika Kuwavutia Wawekezaji katika Maeneo hayo.

Rais Mwinyi ameilezea Sekta ya Biashara kuwa ni eneo jengine Ambalo nchi hizo mbili zinaweza zikashirikiana katika Kuuziana Bidhaa za Ndani.Dk,Mwinyi ameeleza kuwa Bidhaa Nyingi kutoka Afrika Magharibi Zinauzwa nje ya Afrika kuliko zile zinazouzwa katika Ukanda wa Afrika kutokana na Kukosekana kwa Kiunganishi cha Ushirikiano wa Kibiashara.

Rais Dk, Mwinyi amemsisitiza Balozi Celestine Kakele.Kuangalia Uwezekano wa Bidhaa za Zanzibar Ikiwemo Mazao ya Baharini , Mwani na Dagaa kupatiwa Soko katika nchi nyengine za Afrika.

Naye Balozi Kakele amesema Nigeria ni Nchi Kubwa na Ina fursa nyingi ambazo Tanzania ikiwemo Zanzibar zinaweza kushirikiana hususani Uwekezaji katika Biashara na Huduma za Kibenki na Kushauri kuandaliwa Mazingira Wezeshi ya Upatikanaji Viza baina ya Nchi hizo.