Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema nchi inaendelea kuwa katika hali ya amani na utulivu kufuatia kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu, na amewahimiza wananchi kuendelea kuiombea dua ili amani hiyo iendelee kudumishwa.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 15 Machi 2026, alipojumuika na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa katika futari ya pamoja aliyowaandalia.

Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu, Mkoa wa Mjini Magharibi, na kuhudhuriwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi. Pia imehudhuriwa na Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi.