Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameongoza Kikao Kazi kilichowajumuisha Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, kilichofanyika leo tarehe 24 Novemba 2025 Ikulu. Kikao Kazi hicho ni cha kwanza tangu Kipindi cha Pili cha Awamu ya Nane kuingia madarakani.
Rais Dkt. Mwinyi ametoa maagizo kwa Watendaji hao Wakuu na kuwasisitiza kushuka kwa Wananchi kutatua changamoto zinazowakabili, kwa kuwa wananchi wana matarajio na matumaini makubwa kwa Serikali iliyoanza kazi zake rasmi hivi karibuni baada ya kuingia madarakani kwa Awamu nyengine.
