Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuchukua kila juhudi Kuhakikisha Wafanyakazi wanapata stahiki na haki zao za Msingi kwa Mujibu wa Sheria za Utumishi na kanuni ziliopo.Ameyasema hayo katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani 2025 yaliofanyika Viwanja vya Kizimkazi , Wilaya ya Kusini ,Mkoa wa Kusini Unguja.
Dkt,Mwinyi amesema Serikali inatambua na kuthamini Kazi kubwa inayofanywa na Wafanyakazi Kuleta Maendeleo , Kukuza Uchumi na Ustawi wa jamii katika Sekta mbalimbali.Amefahamisha kuwa Ushirikiano Uliopo Baina ya Serikali na Vyama vya Wafanyakazi umekuwa nyenzo Muhimu ya Utatuzi wa Changamoto zinazojitokeza katika Maeneo ya Kazi,Jambo alilolisisitiza kuendelezwa kwani linachangia Kuongeza Ufanisi.
Aidha amewahimiza Wadau Kuendelea na Vikao vya Utatuzi wa Changamoto za Wafanyakazi na kumpa taarifa kila wakati wa hatua wanazochukua Ili kuweka Mazingira mazuri ya Kazi yatakayoleta tija kwa Taifa.Rais Dkt, Mwinyi ameeleza kufarijika na Mchango Mkubwa Unaotolewa na Wafanyakazi walioajiriwa katika Sekta rasmi na wale walio katika Sekta isio rasmi kwani Umefanikisha Utekelezaji wa Mipango mbalimbali ya Serikali na Maendeleo ya Nchi.
Dkt,Mwinyi Ametoa Rai kwa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri kuungana na Serikali kusisitiza Ufanisi na Uwajibikaji katika Maeneo ya Kazi kwani bado wapo Wafanyakazi wasio Waadilifu wanaotanguliza Maslahi Binafsi katika Utekelezaji wa Majukumu yao.Rais Dkt, Mwinyi amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za Kuimarisha Maslahi ya Watumishi ikiwemo Nyongeza ya Mishahara kuwepo kwa huduma ya Afya Ili kuchochea Utekelezaji Bora wa Majukumu Yao kwa dhamira ya kutoa huduma Bora kwa Wananchi.
Akizungumzia Nyongeza ya Mshahara amewaahidi Wafanyakazi kuwa Serikali inaendelea na Mchakato wa kuangalia Uwezekano wa kuongeza Mshahara Baada ya bajeti ya Serikali ya 2025-2026.Rais Dkt, Mwinyi ametoa Wito kwa Wafanyakazi Kuendelea kufanya Kazi kwa Uadilifu, Nidhamu na Uzalendo pamoja na kuwa Walinzi wa Amani iliopo hususani Mwaka Huu wa Uchaguzi Mkuu na kuwasisitiza kushiriki Uchaguzi kwa Amani kwa Maslahi ya Tàifa.
Awali Rais Dkt, Mwinyi aliyafunga Maonesho ya Wafanyakazi na Kuyapokea Maandamano ya Wafanyakazi waliobeba mabango yenye Ujumbe mbalimbali yenye mnasaba na Siku Hiyo ya Wafanyakazi Duniani iliobeba Kaulimbiu inayosema “Wafanyakazi Tufanye Kazi kwa biidii, Tudai haki kwa mujbu wa Sheria na tushiriki Uchaguzi kwa Amani.”