Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi ameungana na Viongozi mbali mbali wa Kitaifa Kuuaga Mwili wa aliekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Cleopa David Msuya aliefariki siku chache zilizopita.
Ibada ya kumuaga Hayati Msuya imefanyika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan aliwaongoza Watanzania.
Akitoa Salamu zake Rais Mwinyi na kwa niaba ya Wananchi wa Zanzibar amemuelezea Hayati Cleopa Msuya kuwa Kiongozi Mahiri aliefanya Kazi kwa Uzalendo kuitumikia nchi yake na Watanzania wamepoteza Kiongozi thabiti na Muumini wa Umoja na Muungano wa Tanzania.
Aidha Dkt,Mwinyi amesema ni Kiongozi aliyeweka mbele Maslahi ya Taifa hasa wakati Tanzania ikikabiliana na Mabadiliko ya Uchumi duniani pamoja na Kuimarisha Diplomasia ya Uchumi.
Rais Dkt, Mwinyi Watanzania Kuyaendeleza Maono ya Hayati Cleopa Msuya kwa kufanya kazi kwa. bidii kuhakikisha Nchi inapiga hatua zaid za Maendeleo.
Hayati Cleopa Msuya alifariki tarehe 7 May 2025 akiwa na Umri wa miaka 94 wakati akitibiwa Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam anatarajiwa Kuzikwa Kijijini kwao Lusangi Mwanga, Mkoani Kilimanjaro siku ya Jumaane ya Wiki ijayo.