Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amejumuika pamoja na Mgeni wake Rais wa Msumbiji Daniel Fransisco Chapo na Ujumbe wake katika Dhifa ya Chakula cha Mchana.Hafla hiyo imefanyika Viwanja vya Ikulu ,Mjini Zanzibar,Wilaya ya Mjini.
Dhifa hiyo pia imehudhuriwa na Mke wa Rais wa Msumbiji Gueta Selemane Chapo na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mariamu Mwinyi.
Viongozi mbalimbali wa Serikali wamehudhuria hafla hiiyo akiwemo Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt, Ali Muhammed Shein ,Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu Balozi Seif Ali Iddi, Jaji Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Shaaban nĂ Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi.
Rais wa Msumbiji Daniel Fransisco Chapo Yupo nchini kwa ziara Maalum yenye lengo la Kuimarisha Uhusiano baina Ya Nchi hizo mbili.