Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi ametoa Mkono wa pole kwa Familia ya Marehemu Charles Martin Barnabas Hilary ,Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu aliefariki Usiku wa kuamkia tarehe 11May 2025.
Dkt, Mwinyi amefika Nyumbani kwa Marehemu Mtaa wa Kibamba CCM, Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam kutoa mkono wa pole kwa Mjane wa Marehemu Sarah Mwakanjuki wana Familia ,jamaa na Marafiki.Rais Dkt, Mwinyi amewataka kuwa na Subira na Uvumilivu kipindi hichi cha Msiba huo Mzito.Marehemu Charles Hilary amefariki akiwa na Umri wa miaka 66, amezaliwa tarehe 22 0ktoba 1959 na kufariki jana.
Rais Dkt, Mwinyi alimteua kushika nyadhifa ya Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano na Habari Ikulu Zanzibar tarehe Tarehe 30 Disemba 2021 na Tarehe O6 Febuari 2023 alimteua kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.