Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar ina fursa nyingi za kiuchumi hususan katika sekta ya Uchumi wa Buluu, ameyasema hayo leo tarehe 19 Dise
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar ina fursa nyingi za kiuchumi hususan katika sekta ya Uchumi wa Buluu, ameyasema hayo leo tarehe 19 Disemba 2025, alipokutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia Mambo ya Nje, Mhe. Dkt. Ngwaru Jumanne Maghembe, pamoja na Naibu Waziri anayeshughulikia Masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. James Kinyasi Millya, waliofika Ikulu Zanzibar, kwa lengo la kujitambulisha.