Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwiinyi amesema Serikali itaendelea kuweka Mazingira Mazuri ya Uwekezaji ili Wawekezaji wengi wenye Mitaji Mikubwa waje kuwekeza Nchini.Dkt,Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 10 Novemba 2025 alipoifungua Rasmi Hoteli ya TEMBO KIWENGWA RESORT iliopo Kiwengwa ,Mkoa wa Kaskazini Unguja. Rais Dkt, Mwinyi amefahamisha kuwa Sekta ya Utalii inaendelea kukua kwa Kasi Kubwa na Tayari Zanzibar imevuka rekodi ya Wacgeni wanoingia Nchini kwani kwa mwezi Oktoba takribani Wageni laki saba na aroubaini na tatu elfu wamewasili.
Ameeleza kuwa hali ya Utulivu na Amani iliokuwepo kabla na Baada ya Uchaguzi Mkuu ni kichocheo kikubwa kinachowavutia Wageni kuitembelea Zanzibar hivi sasa na kuwa azma ya Serikali ya kufikia Wageni Milioni 1 kwa mwaka inaweza kufikiawa hivi karibuni.
Akizungumzia Hoteli hiyo alioifungua Rais Dkt, Mwinyi ameeleza kufurahika kuona Wawekezaji Wazawa wanawekeza Miradi mikubwa yenye tija na kuwataka Wawekezaji wengine kuwekeza zaidi na kukwepa kuwa Watazamaji katika Sekta ya Utalii. Amesema Wawekezaji wa aina hiyo wanachangia dhamira ya Serikali ya kufikia lengo la kuzalisha Ajira laki tatu na hamsini, kwa Vijana kama ilivyoainishwa katika Ilani ya CCM kwani kasi ya Uwekezaji ni kubwa hivi sasa.
Rais Dkt, Mwinyi ameipongeza Menejiment ya Hoteli hiyo kwa Kuwaunga Mkono Wajasirimali wa Eneo la Kiwengwa kwa kupata Soko la Uhakika la Kuuza bidhaa zao katika Hoteli hiyo ikiwemo bidhaa za Baharini , Mbogamboga na bidhaa zengine zinazozalishwa na Wajasimamli wadogo wadogo. Akizungumzia suala la Msamaha wa kodi kwa Wawekezaji amesema Serikali itaendelea na mpango huo ili kuwavutia Wawekezaji zaidi kuwekeza katika sekta mbalimbali.
Waziri wa Wizara ya Kazi na Uwekezaji Mhe, Sharif Ali Sharif amesema Wizara imejipnga vema kuhakikisha Malengo ya Serikali ya kuwa na Uwekezaji wa Miradi yenye Mitaji Mikubwa yanafikiwa kwa kuwa na Usimamizi bora wa Majukumu ya Wirara hiyo yenye dhamana ya Uwekezaji hapa nchini. Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Nd, Saleh Saad amesema Mradi huo wa Hoteli Umegharimu Dola za Marekani Milioni12 na utatoa ajira kwa Wazawa 145 ,Ukiwa na Vyumba vya hadhi ya juu 95 na kuweza kuhudumia Wageni 200 kwa wakati mmoja.
