RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Serikali imeweka mkazo maalum wa kuifungua Pemba kiuchumi kupitia ujenzi wa uwanja wa ndege, bandari na miundombinu ya barabara.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Ujumbe Maalum wa Serikali ya Uingereza, ukiongozwa na Mhe. Kate Osamor (MB), Mjumbe Maalum wa Biashara wa Serikali ya Uingereza kwa Afrika Mashariki.

Katika mazungumzo hayo Rais Dkt. Mwinyi amesema kuwa ujenzi wa miundombinu ya barabara umefikia asilimia 70, sambamba na maendeleo ya ujenzi wa uwanja mpya wa ndege wa Pemba pamoja na bandari.

Akizungumzia kilimo cha mwani ambacho kina mwamko mkubwa kwa wanawake wa Zanzibar, Rais Dkt. Mwinyi amesema kuwa licha ya ongezeko la uzalishaji wa zao hilo, bado bei ya mwani hairidhishi kulingana na juhudi zinazowekwa na wazalishaji. Ameutaka ujumbe huo kuangalia njia bora ya kuwawezesha wazalishaji kwa kuongeza thamani ya zao hilo.