Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 7 (1) cha Sheria ya Kukabiliana na Maafa Namba 1 ya 2015, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bwana Shaaban Seif Mohamed kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Maafa ya Zanzibar.

Kabla ya Uteuzi huo Bwana Shaaban Seif Mohamed alikuwa Msaidizi Mrajis wa Bodi ya Hospitali Binafsi katika Wizara ya Afya.