Salamu hizo zilieleza kuwa wananchi wa Zanzibar wanaungana pamoja na ndugu zao wa Zambia katika kusherehekea siku hii muhimu katika historia ya nchi hiyo ambapo tukio hili la kihistoria lilitokea Oktoba 24 mwaka 1964 ambapo Zambia ilipata uhuru kutoka koloni la Kiengereza.

Aidha,salamu hizo, zilieleza kuwa tukio hilo kubwa, linatoa nafasi ya kuendeleza uhusiano na ushirikiano mkubwa kati ya nchi mbili hizo hatua ambayo itaimarisha zaidi uhusiano katika nyanja za Kitaifa na Kimataifa yakiwemo mashirikiano ndani ya
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika (AU) pamoja na Jumuiya nyenginezo za Maendeleo.

Sambamba na hayo, Dk. Shein alimtakia kiongozi huyo pamoja na familia yake na wananchi wote wa Jamhuri ya Zambia, afya njema na kuwatakia sherehe njema zenye amani na utulivu wananchi wa nchi hiyo.