Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaji, Dkt,Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu Kisiwani Pemba katika Sala ya Eid El Hajj. Sala hiyo imesaliwa Leo Tarehe 27 Mei 2026 katika Msikiti wa Ole Kianga ,Mkoa wa Kusini Pemba.

Wakati huo huo Rais Dkt, Mwinyi amekutana na kusalimiana pamoja na kuwapa Mkono wa Eid Masheikh katika Hafla Maalum iliyofanyika katika Ikulu Ndogo ya Pagali , Mkoa wa Kusini Pemba,  Mapema Alhaji Dkt, Mwinyi alishuhudia Tukio la Uchinjaji wa Ngo’mbe ikiwa ni Sunna katika kusherehekea Sikukuu ya Eid El Adhia.

Waumini wa Dini ya Kiislamu Duniani kote wanasherehekea Sikukuu ya Eid El Adhia kufuatia kukamilika kwa Ibada ya Hijja ambayo ni Nguzo ya Tano ya Uislamu.