Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amewasili Pemba leo Tarehe 26 Mei 2026 kwa ajili kujumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Eid El Hajj pamoja na Baraza la Idd linalotarajiwa kufanyika Kesho.
Alipowasili Uwanja wa Ndege wa Pemba alipokelewa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi, Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe, Hadid Rashid Hadid.
Wakati huo huon Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ametoa Mkono wa Pole kwa Familia ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab kufuatia Kifo cha Ndugu yake Marehemu Bakari Omar Kaab aliyefariki Tarehe 24 Mei 2026 .
Rais Dkt, Mwinyi alifika Nyumbani kwa Familia ya Marehemu Changaweni Mfikiwa kutoa mkono wa Pole kwa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab, Ndugu na jamaa na kuwataka kuwa.na Ustahamilivu na subira wakati huu wa Msiba huo mzito wa kuondokewa na Mpendwa wao.
Marehemu Bakari Omar Kaab alifariki wakati akitibiwa katika Hospitali ya Abdalla Mzee , Mkoani Pemba na kuzikwa Ukutini .
Mwenyezi Mungu amlaze Mahala Pema Peponi. Amin
.jpeg)