Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesitisha Mijadala kuhusu kuongeza Muda wake wa Urais na kusisitiza kusimamia Katiba ya Nchi ipasavyo. Dkt, Mwinyi amesema hivi sasa kupitia Majukwaa mbalimbali ikiwemo Baraza la Wawakilishi kumekuwa na Mijadala na Mapendekezo ya kuongeza Muda wa Uongozi (Urais) badala ya Miaka 10 iliyopo Kikatiba na kueleza kuwa hana nia hiyo na Mjadala huo hauna Tija kwa Nchi Hivi sasa.

Amesema Viongozi wameapa kuilinda Katiba ya Nchi na kutekeleza Majukumu kwa Mafanikio makubwa hivyo ni Vema wakaachwa wakasimamia   eneo hilo kwa Ufanisi na kueleza Kuwa Miaka 4 na nusu ya Uongozi wake iliyobakia ni ya Utekelezaji Mkubwa na Wa kasi zaidi kwa ajili ya Maendeleo ya Nchi na kuagiza kusitishwa kwa Mjadala huo mara moja. Amesema muda huo utakapokamilika Utaratibu wa kupokezana kijiti cha Uongozi Utatekelezwa kwa mujibu wa Sheria na hakuna sababu ya Wananchi kuwa na hofu na Wasiwasi kuhusu suala hilo.

Wakati huo huo Rais Dkt,  Mwinyi amesema Wakati Umefika wa kuondokana na Mashirika ya Umma yanayoendelea kupokea Ruzuku na Ruzuku kutoka Serikalini na kuwa Mzigo kwa Serikali.Rais Dkt, Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 23 Mei 2026 alipolifungua Jukwaa la Wenyeviti na Wakuu wa Taasisi za Umma, Hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa Ndege, Mkoa wa Mjini Magharibi

Dkt, Mwinyi ameeleza kuwa Bado yapo Mashirika ya Umma yanazopkea Kiasi kikubwa cha Fedha za Ruzuku na kulipa Mishahara kutoka Serikalini jambo alilolielezea kuwa limepitwa na Wakati na Serikali haiko tayari kuendelea na Taasisi za aina hiyo pamoja na kueleza kuwa wakati wa Afisi ya Hazina kutoa fedha kwa Taasisi umepitwa na Wakati. Amefahamisha kuwa Serikali itatoa muda kwa Mashirika hayo kujipanga na hatimaye kujiendesha zenyewe kwa faida na zitakazoshindwa Serikali haitakuwa Tayari kuendelea nayo.

Dkt,Mwinyi Ameeleza kuwa Uchumi wa Zanzibar bado una fursa kubwa ya kukua kwa kasi zaidi hivi sasa na kuwataka Wenyeviti ,Wakuu wa Taasisi na Watendaji kwa Ujumla kuangalia fursa za Ukuaji wa Uchumi ziliopo hapa Nchini. Amefahamisha kuwa Bado kuna Changamoto ya kufikia Malengo ya Mapato katika Mashirika ya Umma na Upatikanaji wa Gawio la Serikali hivyo Serikali itaendelea kuweka Mazingira bora ya Usimamizi Makini wa Mashirika ya Umma ili kupata Tija na Matokeo bora.

Aidha Rais Dkt, Mwinyi amesema Mashirika yote ya Umma yana wajibu wa kuhakikisha yanajiendesha yenyewe na hatimaye kutoa Gawio kwa Serikali badala kuwa tegemezi kwa Serikali kama ilivyozoeleka kwa Miaka mingi.Amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Afisi ya Msajili wa Hazina ya kusimamia Taasisi na Rasilimali za Umma pamoja na kuiagiza kuongeza juhudi kuhakikisha Mashirika yote ya Umma yanafanya Vizuri .

Akizungumzia Jukwaa hilo la Wenyeviti na Wakuu wa Taasisi za Umma Rais Dkt, Mwinyi amesema ni Jukwaa muhimu la kujadili Masuala ya Maendeleo na kubaini Changamoto na kuzipatia Ufumbuzi ili Taasisi za Umma ziweze kufikia Malengo na Kueleza kuwa Serikali ipo tayari kupokea Maoni yatakayotolewa na Jukwaa hilo.ili kuleta Maendeleo ya Kiuchumi hapa Nchini

Amefahamisha kuwa Serikali itatoa Msukumo Maalum na Usimamizi bora wa Utendaji katika Mashirika ya Umma pamoja na kuendelea kusimamia Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya 2050 na Uimarishaji na Ujenzi wa Miundombinu ya Bandari ikiwemo Bandari ya Mangapwani ,Uimarishaji wa Viwanja vya Ndege na Viwanja vya Michezo na ,Miundombinu ya Barabara ili kuifanya Zanzibar kuwa Kitovu cha Uchumi endelevu na wa Kisasa .