Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe, Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema Upo umuhimu Mkubwa kwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuimarisha Uhusiano katika nyanja ya Diplomasia ya Uchumi na Uwekezaji.
Rais Dkt, Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 6Julai 2026 alipokutana na Balozi Mpya wa Tanzania Nchini Uganda Mhe, Balozi Meja Jenerali Marco Elisha Gaguti aliyefika Ikulu kujitambulisha na kuaga kabla ya kuelekea katika Kituo cha Kazi.
Dkt, Mwinyi amesema ni wakati sahihi kwa Nchi hizo kuelekea katika kuimarisha Ushirikiiano wa Biashara na Uwekezaji baada ya kuwa na Uhusiano mzuri ili kunufaika na fursa za kiuchumi ziliomo katika kila Nchi . Ameeleza kuwa Kuwepo Uhusiano Mzuri ni jambo la Msingi katika kuendeleza Uchumi miongoni mwa Mataifa hayo.
Rais Dkt, Mwinyi amemsisitiza Balozi Marco kutumia nafasi hiyo kuzitangaza fursa za Uwekezaji na Vivutio vya Utalii wa Tanzania ikiwemo Zanzibar Nchini Uganda hususani kwa Makampuni, Wafanyabiashara na Wawekezaji Wakubwa ili waje kuwekeza Nchini.
Rais Dkt, Mwinyi amemuhakikishia Balozi Marco Ushirikiano Mkubwa katika utekelezaji wa Majukumu yake Mapya ya Kibalozi na kumshauri kuchukua juhudi Maalum za kuwashawishi na kuwaunganisha Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Uganda kutumia fursa ziliopo kuwekeza Tanzania .
Naye Mhe, Balozi Meja Jenerali Marco Elisha Gaguti amemuhakikishia Rais Dkt Mwinyi kufanya kila linalowezekana kutekeleza Majukumu yake kwa Ufanisi na kufuata Muongozo na Maelekezo aliyopokea pamoja na kutekeleza Kimkakati Diplomasia ya Uchumi baina ya Nchi hizo.
.jpeg)