Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na viongozi pamoja na wananchi mbalimbali katika maziko ya Sheikh Said Othman Al Kadiry, aliyefariki dunia tarehe 7 Julai 2026.
Mapema, Rais Dkt. Mwinyi alishiriki Sala ya Jeneza iliyosaliwa katika Msikiti wa Ijumaa wa Tunduni kwa Masharifu, Mkoa wa Kaskazini Unguja leo tarehe 09 Julai, 2026.
Marehemu Sheikh Said Al Kadiry, amefariki akiwa na umri wa miaka 88, alikuwa mwanazuoni mashuhuri wa dini ya Kiislamu, mlezi na msimamizi wa Tariqatul Qadiriyya nchini.
Marehemu amezikwa kijijini kwao Tunduni Mchangani. Mwenyezi Mungu amlaze marehemu mahala pema peponi Amina.
.jpeg)