Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Msarifu wa Benjamin William Mkapa Foundation, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameitaka taasisi hiyo kuendelea kuimarisha huduma za afya na kuboresha maisha ya wananchi kwa kujiimarisha zaidi katika kukabiliana na changamoto za sekta ya afya na mabadiliko ya mifumo ya ufadhili.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 11 Novemba 2026, katika Mkutano wa Mwaka wa Mashauriano na Msarifu wa Benjamin William Mkapa Foundation, uliofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana, Dar es Salaam.
Amesisitiza umuhimu wa kuendeleza ubunifu, kuwajenga wataalamu vijana na kudumisha misingi ya uadilifu, uwajibikaji na utumishi kwa umma iliyoachwa na Hayati Rais Benjamin William Mkapa.
Aidha, amepongeza ushirikiano kati ya Benjamin Mkapa Foundation na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, akibainisha kuwa kuna fursa zaidi za kushirikiana katika sekta ya afya, maendeleo ya jamii na uimarishaji wa rasilimali watu kwa manufaa ya wananchi.
