Katika salamu hizo, Dk. Shein alimpongeza Rais Xi Jinping kwa kutimiza miaka 68 ya Taifa hilo tokea kutangazwa rasmin na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Kikomunisti cha Jamhuri ya Watu wa China Hayati Mao Zedong mnamo Oktoba 1, mwaka 1949.

Salamu hizo zilieleza kuwa wananchi wa Zanzibar wataendeleza umoja na mshikamano walionao kati yao na ndugu zao wa Jamhuri ya Watu wa China kwa lengo la kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya pande mbili hizo.

Aidha, katika salamu hizo, Dk. Shein alimtakia sherehe njema kiongozi huyo wa Jamhuri ya Watu wa China pamoja na wananchi wake wote sambamba na kuendeleza amani na utulivu iliyopo nchini humo pamoja na kuimarisha zaidi mafanikio yaliopatikana katika sekta za uchumi na maendeleo.

Dk. Shein katika salamu hizo, alieleza kuwa katika miaka 68 tangu kuasisiwa kwa Taifa hilo, Jamhuri ya Watu wa China imeweza kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kudumu kati yake na Zanzibar.

Sambamba na hayo, Dk. Shein alimtakia kiongozi huyo pamoja na familia yake na wananchi wote wa Jamhuri ya Watu wa China afya njema, na mafanikio zaidi katika kuuimarisha uchumi wao ambao umekuwa ukiimarika siku hadi siku sambamba na maendeleo yaliopo.