Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali katika maziko ya Bi. Asha Khalid Salum aliyefariki jana.

Marehemu Asha Khalid Salum ni mtoto wa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt. Khalid Salum Mohammed. Alikuwa mfanyakazi wa Wizara ya Kazi na Uwekezaji Zanzibar. Amezikwa kijijini kwao Donge Kitaruni leo, tarehe 06 Machi 2026, kijijini kwao Donge Kitaruni, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Mapema Rais Dkt. Mwinyi alishiriki katika Sala ya Jeneza iliyosaliwa katika Msikiti wa Donge Kitaruni.Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema Peponi. Amina.