Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe ,Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema Matumizi ya Tehama katika Mfumo wa Utendaji wa Mahakama ni Eneo muhimu zaidi linalopaswa kupewa Kipaumbele ili kuharakisha Upatikanaji wa Haki na kuongeza Ufanisi.
Rais Dkt, Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 22 Juni 2026 alipokutana na Jaji Mkuu wa Tanzania ,Mhe, Jaji George Masaju aliyefika Ikulu , Zanzibar kujitambulisha.
Amefahamisha kuwa Mahakama ya Zanzibar ina fursa zaidi za kujifunza katika Eneo hilo kutokana na Mafanikio Makubwa yaliyofikiwa na Mahakama ya Tanzania kwq lengo la kuhakikisha Upatikanaji wa haki za Wananchi kwa Haraka pamoja na kupunguza gharama za Kiutendaji.
Rais Dkt, Mwinyi amesifu Ushirikiano uliopo hivi sasa baina ya Mahakama ya Zanzibar na Mahakama kuu ya Tanzania na kusisitiza kuendelezwa ili kazi za pamoja zinazofanyika baina ya Taasisi hizo ziwe na Tija zaidi.
Aidha amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka Mkazo katika Matumizi ya Tehama na Kuimarisha Miundombinu ya Mahakama katika ngazi zote ili kuwahakikishia Wananchi Upatikanaji wa Haki zao kwa haraka na katika Mazingira yanayopendeza na yalio karibu na Makaazi yao.
Akizungumza Ujenzi wa Miundombinu ya Mahakama Rais Dkt Mwinyi amesema Ujenzi wa Mahakama ya Rufaa Pemba ni hatua nzuri ambayo itatoa fursa kwa Majaji wa Mahakama ya Rufaa kupata Mazingira bora ya kufanya kazi zao Kisiwani humo na kuihakikishia Mahakama Kuu Ushirikiano zaidi.
Naye Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe, George Masaju amesifu Ushirikiano wanaoupata kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mahamama ya Zanzibar na kueleza kuwa Uamuzi wa kuwa na Mahakama Kuu Pemba kuwa ni Uamuzi wa hekima na kuahidi kusimamia ujenzi huo kwa haraka ili Wananchi wapate haki zao katika Mazingira bora pamoja na kuwapunguzia gharama za Ufuatiliaji wa Mashauri yao.
.jpeg)