Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi wapya na kufanya mabadiliko katika baadhi ya Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:-
- Dkt. Idris Muslim Hija ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.
- Bwana Joseph Abdalla Meza ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi.
- Bwana Juma Ali Juma ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Bishara, Viwanda na Masoko.
- Bwana Bakari Haji Bakari ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Zanzibar.
- Bwana Ali Khamis Juma ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko.
- Bwana Iddi Haji Makame ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Fedha na Mipango.
- Kapteni Khatib Khamisi Mwadini ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A, Unguja.
- Bwana Abeid Juma Ali ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete – Pemba.
- Bwana Rashid Hadid Rashid ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake, Pemba.
- Bibi Salama Mbarouk Khatib ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Micheweni – Pemba.
- Uteuzi huo umeanza leo tarehe 22 Septemba 2017.
- Viongozi wote hao wanatakiwa kuripoti Ikulu siku ya Jumapili tarehe 24 Septemba saa 2:30 za Asubuhi tayari kwa kuapaishwa.